• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanasoka wa kimataifa wa Kenya Anthony Akumu atarajiwa kujiunga na Yanga

    (GMT+08:00) 2020-10-22 17:16:49

    Kiuongo wa timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Mkenya, Anthony Akumu, ameibuka na kusema hana tatizo lolote ikiwa atahitajika katika kikosi cha Yanga kwa kuwa yeye anachoangalia ni suala la maslahi mazuri kwake. Akumu ametoa kauli hiyo baada ya Mjumbe wa Kamati ya Usajili Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wao, Injinia Hersi Said, kuweka picha ya kiungo huyo katika ukurasa wake wa Instagram kwa lengo la kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa. Kitendo cha Hersi kuweka picha ya kiungo huyo kwenye akaunti yake ya Instagram na kumtakia kheri ya kuzaliwa, kimeibua maswali mengi na wadau wengi wameona kama Yanga wanaelekea kumsajili nyota huyo. Kiungo huyo alianzia kucheza soka akiwa katika Klabu ya Gor Mahia kisha akatimkia Al Khartoum ya Sudan kabla ya kujiunga na Zesco United ya Zambia na mapema mwaka huu akajiunga na Kaizer Chiefs akichukua nafasi ya aliyekuwa kiungo wa Simba, James Kotei, baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye timu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako