• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Real Madrid yachapwa 3-2 na Shakhtar Donestk kwenye mechi ya klabu bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-10-22 17:17:24

    Katika hali ya kushangaza Real Madrid, wakiwa nyumbani wamekubali kipigo cha magoli matatu kwa mawili dhidi ya klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine kwenye mchezo wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Alfredo Di Stéfano Jijini Madrid. Mabao ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine yalifungwa na Mateus Cardoso Lemos Martins 'Tete' dakika ya 29 na Manor Solomon dakika ya 42, wakati ya Real Madrid yalifungwa na Luka Modric dakika ya 54 na Vinicius Junior dakika ya 59 kabla ya Federico Valverde kufunga dakika ya mwisho ambalo hata hivyo lilikataliwa. Ajabu ya mchezo huo ni kuwa Shaktrar walichezesha timu Bi baada ya kukosi cha kwanza kuwa kwenye karantini kutokana na virusi vya Corona. Kwingineko wachezaji wa Manchester City walishangilia ushindi wa 3-1 dhidi ya FC Porto kwenye mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Etihad. Mabao ya Manchester City yalifungwa na Sergio Aguero kwa penalti katika dakika ya 20, Ilkay Gundogan mpira wa adhabu dakika ya 65 na Ferran Torres dakika ya 73, wakati la Porto lilifungwa na Luis Fernando Díaz dakika ya 14'

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako