• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhusiano kati ya China na Ethiopia watajwa kuwa ni mfano mzuri wa ushirikiano

    (GMT+08:00) 2020-10-22 19:01:34

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw. Dina Mufti, amesema ushirikiano kati ya Ethiopia na China ambao umekuwa na nguvu na wa karibu kwa miaka 50 iliyopita, ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Bw. Mufti amesema tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi mwaka 1970, uhusiano huo umekuwa na mabadiliko makubwa, na umekuwa wa karibu kwenye maswala ya uchumi, siasa, usalama, teknolojia, elimu na kujenga uwezo. Maendeleo hayo makubwa yamehimizwa na uamuzi wa mwaka 2017 wa kufanya uhusiano wa pande hizo mbili kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote.

    Ameongeza kuwa wakati nchi hizo mbili zinakabiliana na tishio la pamoja la COVID-19, ushirikiano kati ya nchi hizo umeimarishwa hata katika sekta ya afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako