• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 114 wafariki na wengine 21 hawajulikani walipo kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo katikati ya Vietnam

    (GMT+08:00) 2020-10-22 19:02:17

    Watu 114 wameripotiwa kufa na wengine 21 hawajulikani walipo kufuatia mafuriko, maparomoko ya udongo na majanga mengine ya asili yaliyotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katikati ya Vietnam tangu mapema mwezi uliopita.

    Idara kuu ya kukinga na kupambana na majanga ya nchi hiyo imesema idadi ya watu waliokufa imeongezeka kutoka watu 111 iliyoripotiwa jana. Hadi kufikia saa moja ya jana jioni watu zaidi ya laki mbili kutoka kwenye kaya zaidi ya elfu 59 walikuwa wamehamishwa kutoka kwenye nyumba zao katika mikoa ya kati. Ng'ombe zaidi ya laki 6.9 pamoja na kuku pia wamekufa kwenye janga hilo.

    Wizara ya viwanda na biashara ya nchi hiyo inaendelea kutoka msaada wa bidhaa muhimu kwenye baadhi ya maeneo huku ikifuatilia kwa karibu bei ya bidhaa hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako