• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali ya kubomoka kwa kanisa nchini Ghana yaongezeka na kufikia 18

    (GMT+08:00) 2020-10-22 19:02:42

    Idadi ya watu waliokufa kutokana na kuanguka kwa kanisa mashariki mwa Ghana imeongezeka na kufikia 18.

    Msemaji wa polisi wa mkoa wa mashariki Bw. Francis Gomado amesema hadi kufikia jana idadi ya watu waliokufa ilikuwa imefikia 14, lakini leo imeongezeka baada ya miili minne kupatikana mapema leo. Pia amesema kazi ya uokoaji imekuwa polepole kutokana na kukosekana kwa vifaa vyenye ufanisi, na watu wamekuwa wakisaidia kwa kutumia vifaa walivyonavyo.

    Pia amesema watu 10 wameokolewa wakiwa hai na sasa wanapatiwa matibabu, na mkuu wa kanisa lililobomoka sasa anashikiliwa na polisi kusaidia uchunguzi.

    Jengo la kanisa la Church of Prosperity lenye ghorofa tatu katika mji wa Akyem Batabi, mashariki mwa Ghana lilibomoka jumanne na waumini kadhaa wamekwama kwenye kifusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako