• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wa Kenya wafaidika na Maonyesho ya Biashara yaliyofanyika mtandaoni Italy

    (GMT+08:00) 2020-10-22 19:41:12

    Wauzaji nje bidhaa wa Kenya walifaidika mno na tukio la hivi karibuni la biashara lililofaynika mtandaoni,hii ikiwa ni dalili ya matarajio ya kufufuka kwa uchumi baada ya athari zilizoletwa na janga la Covid-19.

    Wakati wa Maonyesho ya Biashara ya mtandaoni ya Macfrut Digital 2020 Trade Fair nchini Italy,wafanyabiashara wa Kenya walipata mikataba ya biashara ya $2.1 million(Sh235,224,0000).

    Wafanyabiashara 10 wa kike ambao walionyesha bidhaa zao katika maonyesho hayo ya mtandaoni ya siku tatu waliweza kujadiliana na wadau kutoka pande zote za dunia.

    Maonyesho hayo yalitoa majukwaa kwa wafanyabiashara kuonyesha bidhaa zao na kuhudhuria mikutano na makongamano mtandaoni.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Kukuza Biashara ya mauzo ya nje nchini Kenya Wilfred Marube alisema wamefurahi kuwa hata Covid-19 haikuwazuia wakenya wanaouza bidhaa nje ya nchi kuingiliana na dunia katika barabara za Rimini Italy na kufanya mauzo.

    Alisema shirika hilo litaendelea kutafuta fursa zaidi ili kubadilisha mipango ya kukuza mauzo ya nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako