• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumizi halisi ya uwekezaji kutoka nje nchini China yaongezeka kwa asilimia 5.2

    (GMT+08:00) 2020-10-22 20:04:45

    Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Biashara ya China zinaonesha kuwa, katika miezi 9 iliyopita mwaka huu, matumizi halisi ya uwekezaji kutoka nje ya China yalizidi dola za Kimarekani bilioni 103, na kuongezeka kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.

    Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa mwezi Septemba, matumizi ya uwekezaji kutoka nje ya China yalizidi dola bilioni 14.8, na kuongezeka kwa asilimia 25.1 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo. Hali hii inamaanisha kuwa imani ya wawekezaji wa nchi za nje kwa uchumi wa China inaimarika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako