• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa Umoja wa Mataifa atoa mwito wa kuunga mkono usuluhishi kati ya Sudan na Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2020-10-23 09:21:29

    Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya pembe ya Afrika Bw. Parfait Onanga-Anyanga jana alitoa mwito kwa mataifa duniani kuunga mkono zaidi usuluhishi kati ya Sudan na Sudan Kusini.

    Kwenye Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Bw. Onanga-Anyanga amesema, uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea kuimarishwa, na kutoa fursa ya kufanyika kwa juhudi za amani duniani.

    Amesema, mwanzoni mwa mwezi Septemba, Sudan na Sudan Kusini zilikubaliana kupitia mikataba yao ya ushirikiano ya mwaka 2012 mara moja. Sudan Kusini imetuma ujumbe wa ngazi ya juu kwenda Khartoum tarehe 6 Septemba kufanya mazungumzo kuhusu eneo lenye utatanishi la Abyei.

    Naye naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia opresheni ya Amani Bw. Jean-Pierre Lacroix kwenye mkutano huo amesema, ardhi inayogombaniwa na Sudan na Sudan Kusini bado ni tete, licha ya kuwepo maendeleo kadhaa mazuri.

    Amesema, katika miezi sita iliyopita ushirikiano kati ya Sudan na Sudan Kusini umeimarika, ambapo serikali ya mpito ya Sudan na kundi la upinzani wamesaini makubaliano ya amani tarehe 3 Oktoba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako