Waziri mkuu wa serikali ya mpito wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo kwa simu kuhusu Marekani kuiondoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.
Bw. Pompeo amesema, rais Donald Trump wa Marekani ataanza mchakato wa kuiondoa Sudan kwenye orodha hiyo. Jambo ambalo litaharakisha kuboreshwa kwa uhusiano wa nchi hizo mbili.
Habari zinasema, Marekani itaanza utaratibu wa kuiondoa, ikipata malipo ya Sudan kiasi cha dola za Marekani milioni 335 kwa wahanga wa ugaidi wa Marekani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |