• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yakadiria uchumi wa nchi za Afrika kusini mwa Sahara kuongezeka kwa asilimia 3.1 mwaka kesho

    (GMT+08:00) 2020-10-23 09:27:41

    Shirika la Fedha Duniani IMF limesema, shughuli za kiuchumi katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa Sahara zinatarajiwa kupungua kwa asilimia 3 mwaka huu, lakini zitaongezeka kwa asilimia 3.1 mwaka kesho.

    Shirika hilo pia limesema, makadirio hayo yanakabiliwa na mambo mengi zaidi yasiyokuwa na uhakika, kama vile athari za mlipuko wa COVID-19, upatikanaji wa misaada ya fedha na utengenezaji wa chanjo zenye bei nafuu na zinazoaminika.

    Mkurugenzi wa idara ya mambo ya Afrika ya IMF Abebe Aemro Selassie amesema, nchi za eneo hilo zinakabiliwa na mgogoro mkubwa wa afya na uchumi. Katika miezi kadhaa iliyopita, mgogoro huo umeharibu maendeleo yaliyopatikana na nchi hizo na kuathiri maisha ya mamilioni ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako