• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China huenda ikawa soko kuu la watalii la Kenya baada ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-23 09:33:04

    Bodi ya utalii ya Kenya (KTB) jana ilisema, China huenda ikawa soko kuu la watalii la Kenya baada ya COVID-19.

    Kaimu Mkurugenzi wa maendeleo ya soko wa KTB Bw. Fred Okeyo amesema hivi sasa China ni mojawapo ya nchi kumi za mbele zinazotoa watalii kwa Kenya.

    Bw. Fred Okeyo amesema utalii wa China unatarajiwa kufufuka, na Kenya inajiandaa vya kutosha, ili kuingia kwenye soko hilo kwa wakati mwafaka.

    Bodi ya utalii ya Kenya (KTB) siku hiyo pia imesema, imeanza kutoa mafunzo kwa waongoza watalii ili kuboresha huduma kwa watalii wa kigeni nchini humo.

    KTB imesema waongoza watalii ni muhimu sana, ambao wanaonesha umuhimu wa mabalozi wa chapa za huko, kupitia mawasiliano na wageni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako