• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yatoa wito wa kufanywa upimaji wa haraka katika Afrika ili kuongeza kasi ya vita dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-23 09:39:09

    Shirila la Afya Duniani WHO jana Alhamis lilitoa wito kwa nchi za Afrika kufanya upimaji wa haraka ili kusukuma mbele mapambano dhidi ya janga la COVID-19 barani humo.

    Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Matshidiso Moeti amesema uwezo wa Afrika wa kupunguza ukali wa janga kwa maisha ya watu na miundo mbinu ya afya unategemea upimaji wa haraka kwa watu walio hatarini. Amesema WHO inapendekeza kufanya vipimo vya uchunguzi wa haraka vya antijeni ambavyo vinaweza kubadilisha hali katika mapambano dhidi ya virusi kufuatia kuzidi kusambaa kwa virusi hivyo.

    Nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na uhaba wa vifaa vya upimaji wa COVID-19, ambapo WHO inasema nchi 12 pekee barani Afrika ndio zimefikia kiwango kilichoweka cha kupima watu 10,000 kwa wiki katika mwezi uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako