• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump na Biden kukatana tena uso kwa uso kwenye mjadala wa mwisho wa urais

    (GMT+08:00) 2020-10-23 09:39:52

    Rais wa Marekani Donald Trump na makamu wa rais wa zamani Joe Biden wanakutana tena leo usiku kwenye mjadala wa mwisho wa urais, ambapo watawapa wapigakura wao nafasi ya mwisho ya kujua sera za kila mgombea kutoka chama cha Republican na mpinzani wake wa Democratic ambao watakutana uso kwa uso chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi.

    Mikwaruzano ya hapa na pale na isiyokwisha kati ya kambi mbili za kampeni juu ya kila kitu kutoka sheria za usimamizi wa mjadala hadi ratiba ya mjadala wenyewe, imefanya mchakato kuwa na sintofahamu nyingi kutokana na janga la virusi vya Corona mwaka huu.

    Baada ya wagombea hao kukutana Septemba 29 kwenye mjadala ambao ulikuwa na vurugu tupu ambazo hazikuwahi kushuhudiwa kwenye mijadala iliyopita, Trump alikataa kushiriki kwenye mjadala ulioandaliwa kwa njia ya video, kutokana na kupata maambukizi ya virusi vya Corona, na matokeo yake duru ya pili ya mjadala iliahirishwa na wagombea kufanya mikutano kwenye miji yao mbele ya wapiga kura wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako