• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Nigeria aamuru kusitishwa kwa maandamano dhidi ya ukatili wa polisi

    (GMT+08:00) 2020-10-23 09:40:18

    Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari jana aliwataka vijana wanaoandamana wakipinga ukatili wa polisi, kutoendelea na maandamano yao na kushirikiana vizuri na serikali katika kutafuta ufumbuzi.

    Akitoa wito huo kwenye matangazo ya nchi nzima, Buhari amesisitiza kuwa serikali imeshasikia kilio cha vijana wanaoandamana. Aidha amewaonya waandamanaji kutohatarisha usalama wa taifa na sheria za nchi pamoja na utaratibu wa jamii akisema chini ya hali yoyote ile masuala haya hayatavumiliwa.

    Wito huo wa rais umekuja kufuatia vurugu na uharibifu wa mali za watu binafsi na vituo vya umma zinazofanywa na vijana wenye hasira ambao wanatumia vibaya maandamano ya amani, wakitaka polisi kuacha ukatili wao nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako