• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyota wa klabu ya AZAM apata nafasi kuendeleza kipaji chake Israel

    (GMT+08:00) 2020-10-23 18:30:34

    Kiungo wa klabu ya AZAM FC Novatus Dismas ameuzwa kwenda Klabu ya Macabi Tel Aviv ya Israel kutoka Klabu ya Azam FC. Nyota huyo mwenye tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa msimu wa 2019/20 amepata nafasi hiyo baada ya kufanya vizuri majaribio yake. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit majaribio yake timu ya wakubwa alifaulu jambo ambalo limewafanya mabosi wa Macabi Tel Aviv kurudi mezani na kupewa kijana huyo raia wa Tanzania. Imefahamika kuwa alifanya vizuri majaribio ya kwanza kwa timu ya vijana, na alipokwenda kwenye timu hiyo ya vijana alifanya majaribio tena na kupata nafasi kwenda kwenye timu ya wakubwa, kwa sasa atakuwa ni mali ya Macabi Tel Aviv. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la vijana wa Tanzania kujaribu bahati yao barani Ulaya, hali inayochangia kuinua soka ya Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako