• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba yaonja uchungu wa kufungwa, yachapwa goli moja kwa bila Sumbawanga

    (GMT+08:00) 2020-10-23 18:31:08

    Mabingwa watetezi wa ligi ya Tanzania Simba SC leo wamepoteza mechi ya kwanza ya msimu baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa. Simba SC wanabaki na pointi zao 13 baada ya kipigo cha leo, sasa wakizidiwa pointi tatu na mahasimu wao, Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi sita, wakati Azam FC wanaendelea kuongoza kwa pointi zao 21 za mechi saba. Bao lililoizamisha Simba SC inayofundishwa na Mbelgiji, Sven Vandenbroeck limefungwa na mshambuliaji Samson Mbaraka Mbangula dakika ya 49 akimalizia kazi nzuri ya beki Michael Ismail Mpesa. Tanzania Prisons sasa wamefikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi saba na wanapanda kutoka nafasi ya 14 hadi ya tisa kwenye Ligi Kuu ya timu 18. Yanga SC wameichapa 1-0 Polisi Tanzania bao pekee la kiungo Mkongo, Mukoko Tonombe dakika ya 70 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako