• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cristiano Ronaldo akutwa tena na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-10-23 18:31:32

    Cristiano Ronaldo amepimwa tena na kukutwa na ugonjwa wa corona wakati Juventus ikijiandaa kwa pambano la Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki ijayo dhidi ya Barcelona, kwa mujibu wa ripoti kutoka Italia, kwa sasa Ronaldo amejitenga nyumbani kwake Torino baada ya kupimwa na Covid-19 mnamo Oktoba 13 wakati akiwa na timu ya taifa ya Ureno kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mataifa. Juzi jumatano mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alipimwa tena na kugunduliwa kuwa bado ana virusi hivyo. Fowadi huyo wa Ureno anaweza kuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa Serie A dhidi ya Hellas Verona utakaochezwa jumapili, na pambano dhidi ya Barcelona Oktoba 28. Chini ya sheria za UEFA Ronaldo atahitaji kuwa na vipimo hasi saa 24 kabla ya mchezo wa Barcelona huko Torino.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako