• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM alaani vurugu zilizotokea Guinea baada ya upigaji kura uchaguzi wa rais

    (GMT+08:00) 2020-10-23 18:49:01

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani vurugu zilizotokea nchini Guinea baada ya upigaji kura kwenye uchaguzi wa rais.

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Stephane Dujarric amesema amesikitishwa sana na kupotea kwa maisha na uharibifu wa mali. Pia amezipa pole familia za wahanga na kuwatakia wale waliojeruhiwa wapone haraka.

    Bw. Dujarric pia amesema katibu mkuu ameeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya nchini Cote d'Ivoire kabla ya uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31. Katibu mkuu amelaani matukio ya vurugu yaliyotokea kwenye maeneo ya Bonoua na Dabou ambayo yamesababisha majeruhi kadhaa, na kutoa salamu za rambirambi kwa familia zilizoathiriwa.

    Amewataka wanasiasa na waungaji mkono wao kufanya mazungumzo na kuweka mazingira mazuri ya kufanya uchaguzi shirikishi na wenye amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako