• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika aitaka Afrika kujiandaa kwa utekelezaji wa eneo la biashara huria la Afrika AfCFTA

    (GMT+08:00) 2020-10-23 18:49:22

    Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Afrika Kusini Bw. Cyril Ramaphosa ametoa mwito kwa jumuiya za kikanda za nchi za Afrika RCEs kujiandaa kufanya biashara chini ya makubaliano ya eneo la biashara huria la Afrika AfCFTA litakaloanza kufanya kazi Januari mosi mwaka kesho.

    Rais Ramaphosa amesema hayo kwenye mkutano wa pili wa uratibu wa katikati ya mwaka wa Umoja wa Afrika, akionyesha kuridhika na maendeleo yaliyofikiwa kwenye utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya Afrika ya mwaka 2063, iliyoleta wazo la kuanzishwa kwa eneo la biashara huria la Afrika.

    Amesema kuhimiza uratibu kutafanya nchi za Afrika ziwe karibu kufikia jumuiya ya uchumi ya Afrika inayoendana na misingi ya makubaliano ya Abuja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako