• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China: Ushirikiano wenye usawa kati ya China na Kenya kuleta ushirikiano wa kunufaishana

    (GMT+08:00) 2020-10-23 18:49:44

    Balozi wa China nchini Kenya Bw. Zhou Pangjian amesema ushirikiano wa usawa kati ya China na Kenya utaleta ushirikiano wa kunufaishana.

    Kwenye tahariri iliyotolewa kwenye gazeti la Daily Nation la Kenya, Balozi Zhou amesema ushirikiano wenye matunda na wa pande mbalimbali kati ya China na Kenya ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Balozi Zhou amesema ngazi ya uhusiano kati ya China na Kenya imeinuliwa mara mbili katika siku za hivi karibuni, na sasa uhusiano huo uko katika kipindi kizuri zaidi. Amesema kwa mujibu wa Ruwaza 2030 ya Kenya, ameelewa kuwa ujenzi wa miundo mbinu ni msingi wa mageuzi ya kiuchumi na kijamii nchini Kenya. Amesema China itaendelea kushirikiana na Kenya kuendelea na miradi ya 'ukanda mmoja, njia moja', kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa Beijing wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na yaliyofikiwa kwenye mkutano wa dharura kati ya China na Afrika kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako