• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanariadha Eliud Kipchoge aongeza mkataba na Kampuni Ya Magari Isuzu EA Kwa Mwaka Mmoja Zaidi

    (GMT+08:00) 2020-10-23 18:55:16

    Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za marathon, Eliud Kipchoge, ametia saini mkataba mpya utakaomfanya aendelee kuwa balozi wa mauzo ya magari, bidhaa na huduma zingine za kampuni ya Isuzu East Africa kwa mwaka mmoja zaidi.

    Chini ya maelewano hayo mapya, Isuzu EA itashirikiana na wakfu wa Eliud Kipchoge kuinua hali ya maisha ya wanajamii kwa kuwezesha zaidi kufikiwa kwa miradi ya elimu, ukuzaji wa talanta katika michezo na uhifadhi wa mazingira.

    Kipchoge alirejea Kenya majuzi baada ya kutokea Uholanzi alikoelekea mwishoni mwa mbio za London Marathon zilizoandaliwa mnamo Oktoba 4, 2020.

    Ingawa Kipchoge hakufaulu kuhifadhi ufalme wake jijini London, amefichua mipango ya kuboresha zaidi maandalizi yake kwa minajili ya mashindano yajayo katika mbio za kilomita 42.

    Kipchoge amekuwa akijivunia kutumia magari ya Isuzu D-Max pamoja na mengine mawili aliyotuzwa na Isuzu EA kwa kuibuka mshindi wa mbio za Berlin Marathon mnamo 2018 nchini Ujerumani na kukamilisha kivumbi cha INEOS Challenge 1:59 jijini Austria, Vienna chini ya kipindi cha saa mbili mnamo 2019. Kipchoge alitumia Berlin Marathon mnamo 2018 kuweka rekodi mpya ya dunia ya saa 2:01:39 kwenye mbio za kilomita 42.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako