• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taasisi za fedha zatakiwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi

    (GMT+08:00) 2020-10-23 18:56:23

    Taasisi za fedha nchini Tanzania zimetakiwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi ili kukuza mitaji yao na kuongeza ushindani wa kibiashara dhidi ya wenzao kutoka nje.

    Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitoa rai hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa sekta binafsi waliohudhuria Mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) jijini Dar es Salaam.

    Bi Samia ameongeza kuwa pamoja na ubora wa sera zinazoongoza sekta binafsi, Serikali bado inaamini weledi kwenye utoaji wa huduma za fedha nchini humo ni nguzo muhimu katika kufanikisha ustawi wa sekta ya binafsi.

    Kwa upande wake mwenyekiti wa TPSF, Angelina Ngalula alizipongeza taasisi za fedha nchini humo kwa namna zinavyoshirikiana na sekta binafsi katika kukuza mitaji ya wadau hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako