• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema uchumi wa eneo la Asia na Pasifiki umeanza kufufuka

    (GMT+08:00) 2020-10-23 19:12:35

    Shirika la Fedha la Kimataifa IMF tarehe 21 lilitoa ripoti kuhusu mustakabali wa uchumi wa eneo la Asia na Pacifiki, likisema uchumi wa eneo hilo umeanza kufufuka kutoka hali ya kushuka kutokana na janga la COVID-19, lakini kasi ya kufufuka kwa nchi mbalimbali iko tofauti.

    Shirika hilo limekadiria kuwa uchumi wa eneo la Asia na Pasifiki katika mwaka 2020 utapungua kwa asilimia 2.2, miongoni mwao uchumi wa nchi zilizoendelea utapungua kwa asilimia 4, na uchumi wa masoko yanayoibuka na wa nchi zinazoendelea utapungua kwa asilimia 1.6. Uchumi wa China umefufuka kwa nguvu katika robo ya pili ya mwaka huu, na unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 1.9, na kuifanya China kuwa nchi pekee iliyotimiza ongezeko katika mwaka huu miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako