• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China asisitiza kutatuliwa kwa suala la Abyei kwa njia ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2020-10-23 19:12:53

    Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa balozi Dai Bing jana alitoa hotuba kwenye mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Abyei akizisisitiza pande zote kufanya juhudi kwa pamoja na kutatua suala la Abyei kwa njia ya kisiasa.

    Balozi Dai alisema kutatua suala la Abyei kwa njia ya kisiasa ni maafikiano ya baraza la usalama na kunahitaji kufikiwa kwa makubaliano kati ya Sudan na Sudan Kusini kwa njia ya mazungumzo. China imezipongeza Sudan na Sudan Kusini kwa kuonesha nia nzuri kuhusu hadhi ya mwisho ya Abyei zikiteua maofisa wao wa utendaji huko Abyei. Alisema, Baraza la usalama linapaswa kuheshimu uongozi wa Sudan na Sudan Kusini kuhusu suala la Abyei, kuzihimiza pande hizo mbili kuimarisha mawasiliano na kuanzisha mazungumzo moja kwa moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako