• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taasisi ya utafiti ya Brazil yasema chanjo ya China dhidi ya COVID-19 ni salama zaidi

    (GMT+08:00) 2020-10-23 20:17:06

    Habari zilizotolewa na Shirika la Habari la Uingereza Reuters zinasema, chanjo ya virusi vya Corona iliyotengenezwa na Kampuni ya Kexing ya China inafanya majaribio ya awamu ya tatu nchini Brazil, na matokeo ya awali yamethibitisha kuwa chanjo hiyo ni salama.

    Habari hizo zimemnukuu mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Butantan ya Brazil inayoshughulikia majaribio ya chanjo Bw. Dimas Covas, akisema hadi sasa chanjo hiyo ya CoronaVac imefanyiwa majaribio kwa watu 9,000 wanaojitolea nchini humo, haijaleta madhara, na usalama wake umethibitishwa.

    Mkuu wa jimbo la Sao paulo Bw. João Doria amewaambia waandishi wa habari wa Reuters kuwa, matokeo ya majaribio yamethibitisha kuwa, kati ya chanzo zote zilizojaribiwa, CoronaVac ni salama zaidi, imefanyiwa majaribio kwa watu wengi zaidi, na ina uwezekano zaidi wa kutumika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako