• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano ya kusitisha vita Libya ni hatua muhimu ya kuondoa migogoro barani Afrika

    (GMT+08:00) 2020-10-26 08:30:25

    Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Afrika Kusini Bw. Cyril Ramaphosa, amepongeza kusainiwa kwa makubaliano ya kusimamisha vita nchini Libya na kuyataja makubaliano hayo kuwa ni "hatua muhimu kuelekea kuleta utulivu barani Afrika".

    Kwenye taarifa yake Rais Ramaphosa amesema wanazipongeza pande zote zilizosaini makubaliano ya kudumu, ambayo pia Umoja wa Mataifa umeyataja kuwa ni makubaliano kamili ya kudumu yaliyosainiwa mjini Geneva na wawakilishi wa pande mbili zinazopambana.

    Rais Ramaphosa pia amesisitiza haja ya pande za nje kuheshimu vikwazo vya silaha vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, na kuzitaka zisiingilie mambo ya ndani ya Libya. Rais Ramaphosa pia amesisitiza umuhimu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kushirikiana kuziunga mkono pande za Libya kutafuta suluhisho la kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako