Eneo la maziwa makuu la Afrika liko kwenye mwelekeo wa kufufuka kutokana na mashirika ya kimataifa, mashirika ya kikanda na jumuiya za wenyeji kudhamiria kutatua changamoto na matishio yaliyopo dhidi ya amani na utulivu, na kuimarisha mafanikio yaliyopatikana.
Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa katika eneo hilo Bw. Xia Huang amesema hali hiyo inatokana na wadau muhimu kuongeza juhudi za kutafuta amani na mshikamano.
Kwenye taarifa iliyotolewa jana mjini Nairobi kwenye maadhimisho ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa, Bw. Xia amesema hatua zimepigwa kwenye ushirikiano wa kuvuka mpaka na mafungamano katika ngazi zote, huku wanawake na vijana wakizidi kutambuliwa kama ni sehemu muhimu ya mabadiliko.
Bw Xia pia amesema mkakati wa hivi karibuni uliotungwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuleta amani, kuzuia na kutatua migogoro, unalenga kuhimiza mazungumzo, haki na maendeleo ya watu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |