• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yatangaza rasmi kuanza kwa makubaliano ya kiuchumi na kibiashara na Israel

    (GMT+08:00) 2020-10-26 09:06:48

    Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imetangaza rasmi kuanza kwa makubaliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya Sudan na Israel, ambayo yanalenga kuanzisha ushirikiano kwenye sekta ya kilimo. Wizara hiyo imesema kupitia taarifa kuwa nchi hizo mbili zimefikia uamuzi wa kumaliza uhasama na kurejesha uhusiano wa kawaida kati yao, na kuanza kutekeleza makubaliano ya kiuchumi na kibiashara yanayolenga sekta ya kilimo, kwa ajili ya maslahi ya watu wa nchi hizo mbili.

    Taarifa hiyo pia imesema, Marekani na Israel zimeahidi kuisaidia Sudan kuboresha usalama wa chakula, kuendeleza uchumi na kupambana na ugaidi na itikadi kali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako