• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yatoa wito wa mazungumzo na mwafaka juu ya suala la Bwawa la GERD

    (GMT+08:00) 2020-10-26 09:07:10

    Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Mashariki mwa Afrika (IGAD) limehimiza mazungumzo yafanyike na mwafaka ufikiwe ili kuleta suluhu ya suala la Bwawa kubwa linalojengwa na Ethiopia kwenye mto Nile, GERD.

    Taarifa iliyotolewa na IGAD imezihimiza pande zote zinazohusika kwenye mazungumzo ya suala la bwawa hilo, kuepuka hatua zozote zinazoweza kuongeza mvutano kwenye kanda hiyo. Taarifa pia imesema IGAD ina imani na mchakato unaoongozwa na Umoja wa Afrika kuweza kuleta suluhu inayokubalika kwa Ethiopia, Sudan na Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako