• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkoa wa Xinjiang, China waripoti watu 137 wasio na dalili walioambukizwa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-10-26 09:07:51

    Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China umethibitisha watu 137 wasio na dalili walioambukizwa virusi vya Corona hadi kufikia saa 8 jana alasiri.

    Maambukizi hayo mapya yote yaliripotiwa katika mji wa Kashgar ulioko kusini mwa mkoa huo, baada ya msichana mwenye umri wa miaka 17 kutoka wilaya ya Shufu ya mji huo kuthibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona yasiyoonesha dalili mapema Jumamosi kwenye vipimo vya virusi hivyo vinavyofanyika kila baada ya muda.

    Maambukizi hayo yote yaligunduliwa kwenye kiwanda kimoja wilayani Shufu ambacho wazazi wa msichana huyo wanafanya kazi. Uchunguzi ulioanza Jumamosi umewafuatilia kimatibabu watu waliokuwa karibu na watu hao walioambukizwa na watu wenye hatari kubwa ya kuambukizwa, ambao wote wamewekwa karantini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako