• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Mali watumiana pongezi za maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2020-10-26 09:37:04

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana alitumiana salamu za pongezi na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Mali Bw. Zeini Moulaye kwa kuadhimisha miaka 60 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Bw. Wang Yi amesema Mali ni moja ya nchi za Afrika kusini mwa Sahara zilizoanzisha mapema zaidi uhusiano wa kibalozi na China. Katika miaka 60 iliyopita, pande hizo mbili zimesaidiana kwa dhati na kushirikiana vizuri katika mambo ya kikanda na kimataifa. Amesema, kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona, watu wa China na Mali walisimama kwa pamoja kukabiliana na janga hilo. Bw. Wang Yi anapenda kushirikiana na Bw. Moulaye kutekeleza matokeo yaliyopatikana katika mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, na mkutano maalum wa kilele wa kupambana na janga la COVID-19 kati ya China na Afrika, ili kusukuma mbele uhusiano na ushirikiano kati ya China na Mali upige hatua kubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako