• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuunga mkono utaratibu wa pande nyingi

    (GMT+08:00) 2020-10-26 10:03:19

    Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ametoa hotuba ya kuadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa, na kuhimiza jumuiya ya kimataifa kuunga mkono utaratibu wa pande nyingi na Umoja wa Mataifa, na kuimarisha mshikamano na ushirikiano wa kimataifa.

    Bw. Zhang amesema dunia inakabiliwa na changamoto yanayotokana na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika miaka 100 iliyopita, ambazo ni pamoja na janga la COVID-19, na vitendo vya upande mmoja, kujilinda kibiashara na umwamba, mpango wa kukabiliana na changamoto hizo uliotolewa na rais Xi Jinping wa China ni kufuata mfumo wa kimataifa wenye Umoja wa Mataifa kuwa kiini chake, na utaratibu wa kimsingi wa mahusiano kati ya nchi mbalimbali ambao msingi wake ni katiba ya Umoja wa Mataifa.

    Amesisitiza kuwa China itaendelea kuunga mkono utaratibu wa pande nyingi na Umoja wa Mataifa, ili kushirikiana na jamii ya kimataifa kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako