• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kotoko yamsaini kiungo Mbrazil

    (GMT+08:00) 2020-10-26 15:29:36

    Miamba ya soka ya Ghana, Asante Kotoko, imetangaza kuwa wamekamilisha usajili wa kiungo wa Brazil, Fabio Dos Santos Gama kuelekea msimu wa soka wa 2020/2021. Wamiliki hao wa rekodi ya Ligi Kuu ya Ghana wamekuwa wakifanya kazi katika dirisha la uhamisho kwa nia ya kukusanya kikosi bora kwa mashindano yanayokuja. Kotoko inajiandaa kutambulisha kikosi tofauti katika msimu wa soka wa 2020/2021 baada ya kuondoa wachezaji 15 kutoka msimu uliopita. Wakati wa msimu wa 2019/2020, wababe hao wa Ghana walifurahia msimu mzuri, lakini, hawakuweza kuendelea katika mashindano yoyote ya klabu ya CAF licha ya kushiriki katika Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako