• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe azishukuru China na Russia kwa kuunga mkono nchi hiyo kuondolewa vikwazo

    (GMT+08:00) 2020-10-26 16:10:00
    Rais wa Zimbabwe azishukuru China na Russia kwa kuunga mkono nchi hiyo kuondolewa vikwazo

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amezishukuru China na Russia kwa kusimama pamoja nayo katika wito wake wa kutaka kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi bila masharti.

    Katika hotuba ya kuadhimisha Siku ya Kupinga Vikwazo inayoadhimishwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), rais Mnangagwa amezishukuru nchi hizo mbili, SADC, Umoja wa Afrika na nchi nyingine duniani kwa kuiunga mkono Zimbabwe. Amesema nchi hizo sio tu ziliisaidia Zimbabwe katika kupambania uhuru wake, lakini pia zimeisaidia kulinda ukamilifu wa ardhi yake dhidi ya mashambulizi ya wabaya wake.

    Rais Mnangagwa pia ameushukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuchukua hatua kadhaa ili kurejesha uhusiano wa kawaida na Zimbabwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako