• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zapata mafanikio katika kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-26 16:16:08

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Tedros Ghebreyesus amesema, kazi za kudhibiti mlipuko wa virusi vya Corona barani Afrika kwa sasa zinaendelea vizuri, na idadi ya kesi mpya za virusi hivyo barani humo imeanza kupungua.

    Habari zinasema, mafanikio hayo ni kutokana na nchi za Afrika kuongeza uwezo wa upimaji, kudhibiti na kutibu, ambapo mpaka sasa kuna maabara 750 barani humo zinazopima virusi hivyo, na watu zaidi ya milioni 15 wamepimwa.

    Idadi ya vitanda vya hospitali barani Afrika zinazoweza kutibu wagonjwa wa COVID-19 imeongeza kutoka elfu 13 mwezi Aprili hadi elfu 43 mwezi Agosti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako