• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono nchi za Afrika kuzitaka nchi za magharibi kuondoa vikwazo haramu dhidi ya Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2020-10-26 18:22:44

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesisitiza kuwa China inaunga mkono nchi za Afrika kuzitaka nchi za magharibi kuondoa mapema vikwazo haramu dhidi ya Zimbabwe.

    Bw. Zhao amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo. Amesema Mkutano wa 39 wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika mwaka jana uliiweka tarehe 25 Oktoba kuwa "Siku ya Kupambana na Vikwazo", ikizitaka nchi na mashirika kadhaa ikiwemo Marekani kuondoa mapema vikwazo haramu dhidi ya Zimbabwe. Amesema jana ilikuwa maadhimisho ya pili ya Siku hiyo, ambapo nchi za Afrika zimetoa wito huo wenye msimamo wa haki kwa mara nyingine.

    Pia amesisitiza kuwa China siku zote inaunga mkono kithabiti nchi za Afrika ikiwemo Zimbabwe kupambana na nguvu za nje kuingilia mambo ya ndani, na kutafuta maendeleo kwa kujitegemea. Pia inaona kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kufanya kazi ya kiujenzi katika kuisaidia Afrika kulinda utulivu na kupata maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako