• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Misri atangaza tena hali ya hatari kwa miezi mitatu

    (GMT+08:00) 2020-10-26 19:10:51

    Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ametangaza tena hali ya hatari nchini humo kwa miezi mitatu zaidi kuanzia leo Jumatatu.

    Gazeti la Ahram linalomilikiwa na serikali ya nchi hiyo limechapisha tangazo hilo linalosema, vikosi vya ulinzi na polisi vitachukua hatua zinazotakiwa kupambana na ugaidi na wafadhili wake, kudumisha usalama wa nchi, kulinda mali za umma na binafsi, na kulinda maisha ya raia wake.

    Kutokana na katiba ya Misri, uamuzi wa rais wa kutangaza tena hali ya hatari nchini humo ni lazima upitishwe na bunge la nchi hiyo.

    Kwa mara ya kwanza, rais Al-Sisi alitangaza hali ya hatari ya miezi mitatu mwezi April mwaka 2017, baada ya mashambulizi ya mabomu katika makanisa mawili yaliyoko mikoa ya kaskazini ya Gharbiya na Alexandria ambayo yalisababisha vifo vya watu 47 na kujeruhi wengine zaidi ya 120.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako