• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UGANDA YAPIGA HATUA KATIKA UCHIMBAJI WA MAFUTA

    (GMT+08:00) 2020-10-26 20:24:52

    Kampuni ya kuchimba mafuta ya Tullow imepata ruhusa kutoka Serikali ya Uganda,kuuza mgao wake wa machimbo ya mafuta katika eneo la ziwa Albert kwa kampuni ya Ufaransa ya total.

    Hatua hiyo inatarajia kutoa fursa ya kuanza kwa hatua ya mwisho ya uwekezaji katika kuchimba na kusafirisha mafuta ya Uganda kwa soko la kimataifa, ikiwemo ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta hayo kutoka Hoima Uganda hadi Tanga, Tanzania.

    Katika taarifa kwa vyombo vya habari, kampuni ya Tullow ilisema kwamba Serikali ya Uganda na mamlaka ya kukusanya ushuru Uganda URA, zilifikia makubaliano kuhusu namna ya kulipa ushuru kutokana na kuuza kwa vifaa vyake kwa kampuni ya Total. Kampuni ya Tullow itapokea dola milioni 500 katika hatua ya kwanza na dola milioni 75 maamuzi ya uwekezaji ya mwisho yatakapochukuliwa kuhusu mradi huo wa kuchimba mafuta.

    Kampuni ya Tullow pia ina haki ya kupokea sehemu ya pesa zitakazopatikana katika awamu ya kwanza ya uchimbaji mafuta hayo.

    Tangu mwaka 2016, Uganda imekuwa ikikumbana na changamoto kadhaa za kisheria, kuhusiana na uchimbaji mafuta yake yanayotarajiwa kuelekea dola bilioni 3.5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako