• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Nigeria lawaua majambazi 38 kaskazini magharibi mwa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2020-10-27 08:50:15

    Jeshi la Nigeria limethibitisha kuwa mpaka sasa majambazi 38 wameuawa kwa mwezi huu kwenye operesheni mbalimbali zilizofanywa na vikosi vya serikali kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

    Msemaji wa jeshi hiyo Bw. Benard Onyeuko amesema kupitia taarifa kuwa jumla ya wengine 198, wakiwemo washirika wao, walikamatwa kwenye Operesheni ya 'Sahel Sanity' iliyofanyika kwenye eneo hilo, na mateka 108 pia waliokolewa kutoka kwa majambazi hao kwenye operesheni hiyo.

    Taarifa imesema kuwa operesheni ya 'Sahel Sanity' inalenga kutokomeza ujambazi, wizi wa mifugo, utekaji nyara na mauaji ya raia wasio na hatia kwenye eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako