• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachangia tani 1,500 za mchele kuiunga mkono Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2020-10-27 09:15:09

    Serikali ya China imetoa msukumo kwa mchakato wa kisiasa wa Sudan Kusini kwa kutoa mchango wa tani 1,500 za mchele kusaidia mchakato wa kuunganisha majeshi.

    Mchango huo uliotolewa kwa kamati ya mpito ya taifa NTC utatumika kwa ajili ya chakula kwa maelfu ya wanajeshi walikusanywa kwenye vituo mbalimbali.

    Akiongea wakati wa makabidhiano ya mchango huo, Waziri wa ujenzi wa amani wa Sudan Kusini Bw. Stephen Paul, ameishukuru serikali ya China na watu wake kwa mchango huo, na kusema utasaidia kuharakisha mchakato wa kuunganisha majeshi ya Sudan Kusini.

    Balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Huang Ning, amesema mbali na mchango huo, tangu mwaka jana China imetoa mchango wa mahema 2,500, mablanketi elfu 50 na tani 3,000 za mchele.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako