• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majeshi ya Somalia yawaua wapiganaji wanne wa kundi la Al-Shabaab kusini mwa Somalia

    (GMT+08:00) 2020-10-27 09:15:31

    Wapiganaji wanne wa kundi la Al-Shabaab jumapili iliyopita waliuawa kwenye mapambano makali yaliyotokea kwenye mji wa Qansah Dhere katika mkoa wa kusini wa Bay.

    Mkuu wa mji wa Qansah Dhere Bw. Abdi Ibrahim amesema wapiganaji hao walishambulia msafara wa magari uliokuwa umebeba wanajeshi wa serikali na kuelekea kwenye kambi ya jeshi la serikali katika mji huo. Amesema walifanikiwa kuwaua wapiganaji wanne wa kundi hilo, na mwanajeshi mmoja wa serikali pia aliuawa.

    Kundi la Al-Shabaab lenye uhusiano na kundi la Al-Qaeda lilitimuliwa mjini Mogadishu mwaka 2011, lakini bado linashikilia ngome zake katika maeneo ya vijiji kwenye mikoa ya kusini na kati, na lina uwezo wa kufanya mashambulizi na kuweka mabomu ya kutegwa ardhini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako