• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wasema vijana wa Afrika wanakabiliwa zaidi na madhara ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-27 09:15:51

    Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika inasema vijana wa Afrika wenye umri wa chini ya miaka 35, ambao ni asilimia 75 ya watu bilioni 1.2 barani Afrika, wanakabiliwa zaidi na madhara yanayotokana na virusi vya Corona.

    Taarifa hiyo imesema kutokana na kuwa vijana wa Afrika ni sehemu muhimu ya ajenda ya maendeleo ya Afrika, matokeo ya mapambano ya virusi hivyo kwa vijana yana madhara ya muda mrefu kwao na kwa mwelekeo wa bara la Afrika.

    Taarifa imesema mbali na elimu yao kukwamishwa kwa miezi mingi kutokana na wengi wao kutojiunga na mtandao wa internet, COVID-19 pia imetishia kazi zao, hasa kwa vijana wenye ujuzi wa chini, wajasiriamali vijana na vijana kwenye sekta binafsi ambao hawawezi kupata ruzuku kutoka serikalini. Taarifa pia imesema madhara ya COVID-19 yatakuwa ya muda mrefu kuliko virusi vya Corona vyenyewe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako