• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM: Ushirikiano wa kimataifa ni njia pekee ya kushinda COVID-19 na mabadiliko ya tabianchi

    (GMT+08:00) 2020-10-27 09:20:52

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema ushirikiano wa kimataifa ni njia pekee ya kushinda janga la COVID-19 na mabadiliko ya tabianchi.

    Bw. Guterres amesema hayo akihutubia maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa, kuwa hivi sasa kazi za Umoja wa Mataifa ni muhimu kuliko wakati wowote wa zamani, jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya juhudi za pamoja, ili kuzuia migogoro, na kutimiza malengo makuu ya kuhimiza maendeleo endelevu, kulinda haki za binadamu na kulinda dunia yetu.

    Umoja wa Mataifa ulianzishwa Tarehe 24 Oktoba mwaka 1945, baada ya Katiba yake kuanza kutekelezwa. Mwaka 1947, Baraza Kuu la Umoja huo lilipitisha azimio, na kuifanya tarehe 24, Oktoba ya kila mwaka iwe Siku ya Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako