• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi wa WHO asema kulifanya janga la COVID-19 kuwa la kisiasa kutasababisha vifo vya watu wengi zaidi

    (GMT+08:00) 2020-10-27 09:33:31

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani Bw. Tedros Ghebreyesus amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona duniani katika wiki iliyopita imefikia kiwango cha juu kabisa tangu kutokea kwa janga hili, na idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa na watu waliopelekwa hospitali katika nchi nyingi za kaskazini mwa Ikweta imekuwa ikiongezeka. Katika nchi za Ulaya na Amerika kaskazini, vyumba vya wagonjwa mahututi vimekuwa vinafanya kazi kuzidi uwezo wake.

    Bw. Tedros amesema kama viongozi wakiweza kuchukua hatua kwa haraka na kwa mpango, kuenea kwa virusi kutazuiliwa. Pia ametahadharisha kuwa kulifanya janga la COVID-19 kuwa la kisiasa kutasababisha vifo vya watu wengi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako