• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika waihimiza Nigeria ichukue hatua za amani ili kupunguza mvutano nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-10-27 13:27:17

    Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya wanawake, amani na usalama Bi. Bineta Diop, ameihimiza serikali ya Nigeria ichukue mara moja hatua za amani za mazungumzo ili kupunguza mvutano unaozidi kupambana moto nchini humo, kufanya uchunguzi kuhusu mauaji, na kuwafikisha wahusika mahakamani.

    Bi. Diop amewasilisha salamu za pole kwa familia za marehemu, pia ameahidi kuunga mkono juhudi za Nigeria na kufanya ushirikiano na shirika la Mtandao wa viongozi wa wanawake wa Afrika nchini Nigeria (AWLN), na kuongeza mchango wa wanawake katika kutafuta suluhisho la kudumu, ili kuhakikisha amani na usalama wa watu wa Nigeria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako