• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Spurs wapata ushindi mlaini dhidi ya Clarets ugenini

    (GMT+08:00) 2020-10-27 15:46:56

    Mechi kati ya Burnley na Tottenham Hotspur iliyochezwa jana usiku iliwashuhudia wenyeji wa London wakiendeleza ubabe wao katika Ligi Kuu huku wakisajili ushindi wa 1-0 ugani Turf Moor. Bao la Son Heung-Min kunako dakika ya 76 ya mchezo ndilo liliweka mwanya kati ya timu hizo mbili. Spurs walikuwa makini kurejea katika mtindo wao wa ushindi baada ya kulazimishiwa droo ya 3-3 na West Ham United katika mchezo wao wa awali wa ligi. Ushindi wa jana usiku uliwapandisha hadi kwenye nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 11, pointi moja nyuma ya Leicester City ambao wanashikilia nafasi ya nne. Burnley bado wako kwenye hatari ya kuondolewa kwenye Ligi Kuu baada ya kuanza vibaya msimu mpya wakiwa na pointi moja pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako