• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Fury amkataa Deontay Wilder

    (GMT+08:00) 2020-10-27 15:47:22

    Bondia Tyson Fury ambaye ni bingwa wa taji la WBC la uzani wa juu 'heavy weight' atapambana na mpinzani wake atakayewekwa hadharani hivi karibuni katika ndondi za haiba kubwa zitakazopigwa jijini London, Uingereza Disemba 5, 2020. Promota wa Fury, Frank Warren amesema kwamba Fury amefutilia mbali mpango wa kuchapana na Deontay Wilder wa Marekani kwa mara ya tatu mnamo Disemba 2020, na tayari amepata mshindani mpya. Fury alimchapa Wilder kwa 'Knock-Out' katika raundi ya saba ya masumbwi yaliyoandaliwa jijini Las Vegas, Marekani Februari 2020. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Fury kumzidi maarifa Wilder baada ya wawili hao kuambulia sare mwaka 2018 jijini Los Angeles.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako