• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BASKETBALL: Rais wa TBF atoa neno, Kurasini Heat mabingwa NBL

    (GMT+08:00) 2020-10-27 15:47:41

    Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Phares Magesa, amewapongeza mabingwa wa michuano ya ligi ya taifa ngazi ya vilabu, Kurasini Heat kwa kuleta mapinduzi na kupata mafanikio katika mchezo huo kwa kuzipiku timu kongwe kama Vijana, Pazi na Savio. Kurasini Heat ambao ndio mabingwa wa RBA, walifanikiwa kutwaa ubingwa wa taifa ngazi ya vilabu, baada ya kuibuka washindi kwa alama 76- 59 dhidi ya Oilers katika fainali iliyochezwa uwanjani Don Bosco, Upanga jijini Dar es salaaam. Bingwa wa ligi ya taifa vilabu bingwa NBL Wanaume atawakilisha Tanzania katika mashindano ya kombe la klabu bingwa ya Afrika (Basketball Africa League - BAL).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako