• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Ikulu ya Marekani asema Marekani haitadhibiti janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-27 16:22:24

    Mkuu wa Utumishi katika Ikulu ya Marekani Mark Meadows amesema kuwa, Marekani haitadhibiti kuenea kwa virusi vya Corona, wakati maambukizi yakiendelea kuongezeka nchini humo.

    Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la CNN kuhusu hali ya taifa, Meadows amesema nchi hiyo haitadhibiti janga hilo, bali itadhibiti ukweli kwamba wanapata chanjo, kutibu na maeneo mengine ya udhibiti.

    Meadows amesema, virusi hivyo vinaambukiza sawa na mafua, na kuongeza kuwa kinachohitajika ni kuhakikisha kuwa hatua za udhibiti zinawekwa, iwe ni kutibu ama chanjo ili kuhakikisha kuwa watu zaidi hawapotezi maisha kutokana na virusi hivyo.

    Takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha John Hopkins zimeonyesha kuwa, mpaka kufikia jana asubuhi, Marekani ilikuwa na kesi zaidi ya 8,700,000 za maambukizi ya virusi vya Corona, huku zaidi ya watu 225,700 wamefariki kutokana na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako