• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yachunguza tukio la waandamanaji kupigwa risasi

    (GMT+08:00) 2020-10-27 18:30:02

    Gavana wa Jimbo la Lagos nchini Nigeria, Babajide Sanwo-Olu amesema, uchunguzi unaendelea kuwagundua watu waliohusika katika tukio la shambulizi la risasi Jumanne iliyopita katika soko la Lekki Toll.

    Katika taarifa yake ambayo Shirika la Habari la China Xinhua lilipata nakala yake, Gavana huyo ameahidi kuwa uchunguzi wa kina utafanywa na Jopo la uchunguzi la Lagos kuhusu kilichotokea na watu wanaoshukiwa kufanya kitendo hicho watawajibishwa. Amesema watu wanadai kuwa ndugu na marafiki zao wameuawa, hivyo kazi ya Jopo hilo ni kuhakiki habari hizo, na kwa wanafamilia kuwatambua maofisa waliowajibika na kitendo hicho.

    Jumla ya watu 69, wakiwemo raia, polisi na wanajeshi wameuawa wakati wa maandamano yaliyofanyika nchini Nigeria kupinga ukatili wa polisi katika siku zilizopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako